Shirika la Msalaba Mwekundu limesema watu wenye silaha wamewauwa zaidi ya watu 168 katika jimbo la Kwara nchini Nigeria. Hayo ni miongoni mwa mashambulizi mabaya kuwahi kutokea nchini humo katika miezi ya hivi karibuni.

Mashambulio hayo yalifanyika siku ya Jumanne jioni katika kijiji cha Woro baada ya jeshi kufanya operesheni kwenye eneo hilo dhidi ya makundi ya kigaidi. Hali ya ukosefu wa usalama nchini Nigeria inafuatiliwa kwa karibu katika miezi ya hivi karibuni tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipodai kwamba  mauaji ya kimbari ya Wakiristo yanaendelea nchini humo.

Madai hayo hayo yanapingwa vikali na serikali ya Nigeria na hata wataalamu wengi wenye misimamo huru, ambao wanasema ukosefu wa usalama nchini Nigeria haubagui dini wala kabila, unadhuru maisha ya Wakristo na Waislamu pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *