Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Riziki Shemdoe amekutana na uongozi wa NMB Bank kujadili maboresho ya mchakato wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vinavyonufaika kupitia benki hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vikundi vyenye sifa stahiki vinapata mikopo kwa wakati, ili kuongeza tija ya mpango huo na kuimarisha ustawi wa walengwa.

Ujumbe wa Benki ya NMB umeongozwa na Mkuu wa Biashara ya Serikali wa benki hiyo, Vicky Bishubo, ambaye amesema taarifa zinazodai kuwa walengwa wanatakiwa kuweka dhamana ili kupata mikopo ya asilimia 10 si za kweli, akisisitiza kuwa mikopo hiyo hutolewa bila dhamana na kwa masharti nafuu.

Katika hatua nyingine, Prof. Shemdoe ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya afya ya msingi na elimu ya msingi, pamoja na kushirikiana katika kurahisisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa walengwa.

#AzamTVpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *