Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameilaani Urusi kwa kushambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine.

Zelenskyy alifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Februari 3 huko Kyiv na Katibu Mkuu wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Kaskazini mwa Atlantiki, NATO Mark Rutte aliyetembelea nchi hiyo, kufuatia shambulio la usiku kucha.

Serikali ya Ukraine inasema takribani makombora 70 na ndege zisizo na rubani 450 zililenga miundombinu ya kupasha joto jijini Kyiv na Kharkiv na Dnipro katika upande wa mashariki. Kampuni ya nishati inaelezea shambulio hilo kama kubwa zaidi hadi sasa mwaka huu.

Zelenskyy alisema Urusi kiuhalisia inategemea vita tu, akiishutumu nchi hiyo kwa kuanzisha shambulio hilo wakati maafisa waandamizi kutoka Ukraine, Urusi na Marekani wakipangiwa kukutana Februari 4 ikiwa ni mapema zaidi.

Shambulio hilo lilitokea baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema Januari 29 kwamba alimuomba Rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha mashambulizi kwa wiki moja na kwamba alikubali.

Wizara ya ulinzi ya Urusi iliweka taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba shambulio hilo lilikuwa jibu la kile inachokiita mashambulizi ya kigaidi ya Ukraine kwenye vituo vya raia katika eneo la Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *