
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amehudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Februari 5, 2026 katika Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa wanachama wa CCM kutekeleza wajibu wao wa msingi na wa kudumu kwa kuhakikisha chama kinaendelea kuwa cha Watanzania wote na kuwa ndio kimbilio lao.
Dkt. Nchimbi amesema kuwa kila mwanachama na kiongozi wa CCM anatakiwa kutafakari matendo yake na namna yanavyochangia maendeleo, kuimarisha umoja na mshikamano wa chama pamoja na Taifa kwa ujumla.