Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, baada ya mawaziri kutoka pande zote mbili kusaini mikataba 18 inayohusisha ulinzi, utalii, afya na kilimo, kwamba biashara ya pande mbili imefikia karibu dola bilioni 9, na kuifanya Misri kuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa Uturuki katika bara la Afrika.

Al-sisi alisema wamekubaliana kuhusu hitaji la kutekeleza awamu zote za makubaliano ya Gaza yaliyosimamiwa na Marekani, wakikataa majaribio yoyote ya kukwepa au kuzuia utekelezaji wa mpango wa amani wa Rais Donald Trump. Viongozi hao waliongeza kuwa msaada wa kimataifa unahitajika kwa ajili ya kupona mapema na ujenzi upya huko Gaza.

Kuhusu Sudan, Al-sisi alisema pande zote mbili zinataka kuona usitishaji mapigano kuruhusu misaada ya kibinadamu ambao utaidia kufikisha mwisho mapigano na kutoa njia pana ya makubaliano ya kisiasa.

Erdogan alisisitiza umuhimu wa diplomasia, akisema kuingiliwa kwa kigeni kunaleta hatari kubwa kwa eneo lote na kwamba mazungumzo yanabaki kuwa njia inayofaa zaidi ya kushughulikia migogoro na Iran.

Viongozi wote wawili pia walisisitiza uungaji mkono kwa kuheshimiwa mipaka na uhuru wa Somalia huku kukiwa na msuguano mkubwa wa kikanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *