#HABARI: Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulidi, amewataka wananchi kupuuza chokochoko za watu wanaoishi nje ya nchi wanaolenga kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini.

Akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 49 ya CCM yaliyofanyika kijijini Kinyagigi, Singida, Mhe. Maulidi ambaye pia ni Mlezi wa CCM mkoani humo, amesisitiza umuhimu wa mshikamano huku akivishwa mavazi ya jadi na wazee wa Singida kama ishara ya kumkaribisha na kumtambua kama mkazi wa mkoa huo.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana mkoani humo chini ya Serikali ya awamu ya sita, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Martha Mlata, akiahidi kuendelea kulinda utulivu uliopo. Aidha, Mwenyekiti wa CCM Singida Vijijini, William Nyalandu, ametumia fursa hiyo kuwasilisha ombi la rasmi la ujenzi wa barabara ya lami ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *