Zaidi ya watu milioni 3 wamerejea nyumbani kwa nhcini Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM wengi wa watu wanaorejea nyumbani wamekuwa wakienda moja kwa moja kwenye maeneo yao ya awali au maeneo ya jirani kuanza maisha upya.
Familia zinarudi kwenye uharibifu, karibu miaka mitatu katika mzozo. Maeneo mengi ya kurudi yana uharibifu mkubwa wa makazi, huduma za msingi, na miundombinu muhimu.
Familia zinarejea kwenye hali uharibifu wa kiwango cha juu baada ya takribani miaka mitatu ya vita
Mazingira yako taabani, nyumba zimebomolewa, huduma za msingi zimesambaratika, na miundombinu muhimu inahitaji ukarabati mkubwa.
Wengi waliorejea walikuwa wakimbizi wa ndani nchini humo hapo awali. Takriban 83% ya waliorejea walitoka ndani ya Sudan, wakati 17% walirejea kutoka nje ya nchi.
Watu wengi wanaorejea walikuwa wakimbizi wa ndani
Asilimia 83 ya watu wanaorejea wametokea ndani ya Sudan, huku asilimia 17 pekee ndio wanaotokea nchi jirani na kurejea makwao.
Maeneo ya kurudi yanahitaji makazi kwa dharura na ujenzi upya.
Jamii zinazowapokea ndizo zinazobeba mzigo mkubwa wa kutoa msaada na huduma
IOM inasema familia zinarejea zikiwa na mizigo kidogo na zingine bila chochote na zikiwa uwezo mdogo sana wa kifedha, jambo linalozidisha hatari ya kupata madhara kutokana na kulemewa kwa miundombinu.
Uhamishaji bado unazidi kuwa mbaya katika maeneo yenye migogoro.
Maeneo wanayofikia yanahitaji kujengwa upya ili kufaa kwa makazi
Maeneo hayo yanahitaji ujenzi wa dharura wa makazi, mifumo ya maji, shule, na vituo vya afya ambavyo kwa sasa vimezidiwa na wagonjwa.
Maelfu bado wamenaswa katika miji ya Kordofan, Darfur na El Fasher, ambako vita vinaendelea kupamba moto.
Hali ya watu kufurushwa bado ni mbaya katika maeneo yenye migogoro
Wakati wakirejea nyumbani, ghasia zimezidi kuongezeka huko jimboni Darfur na Kordofan na kusababisha maelfu ya wakimbizi hususan wa ndani kuongezeka.
IOM inatoa makazi na maji miongoni mwa huduma nyingine muhimu kwa maeneo yanayofikika.
Watoa huduma wa IOM wanaonesha juhudi
Timu za Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji (IOM) zimekuwa zikitoa hifadhi, maji, na huduma nyingine muhimu katika maeneo yote yanayoweza kufikika kwa usalama.
Sudan bado ni janga kubwa zaidi la watu kuhama makazi yao. Hata kwa kurudi, zaidi ya watu milioni tisa wamesalia kuwa wakimbizi wa ndani nchini.
Machafuko nchini Sudan bado ni chanzo kikubwa cha wakimbizi duniani
Zaidi ya watu milioni 9 wamebaki kuwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan licha ya baadhi ya familia kuanza kurejea makwao na mamilioni wengine wamekimbilia nchi jirani.
Sudan bado ni janga kubwa zaidi la watu kuhama makazi yao. Hata kwa kurudi, zaidi ya watu milioni tisa wamesalia kuwa wakimbizi wa ndani nchini.
Msaada unahitajika ili kujenga upya maisha yao
Msaada zaidi unahitajika sasa ili kuwasaidia kujenga upya maisha yao kwani mahitaji yamezidi rasilimali zilizopo nchini humo.