Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi amesema mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yatafanyika Ijumaa nchini Oman, huku mvutano kati ya nchi hizo ukiendelea kuwa mkubwa kufuatia msako mkali wa Tehran dhidi ya maandamano ya kitaifa mwezi uliopita.

Tangazo hilo la jana Jumatano la waziri Araghchi lilikuja baada ya saa kadhaa za dalili kwamba mazungumzo yaliyotarajiwa yalikuwa yanayumba kuhusu mabadiliko katika muundo na maudhui ya mazungumzo hayo.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump, ametuma onyo kali kwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei kabla ya mazungumzo hayo, akisema anapaswa kuwa na wasiwasi sana.

Utawala wa Trump umethibitisha kwamba Marekani itashiriki katika mazungumzo ya ngazi ya juu na Iran nchini Oman badala ya Uturuki kama ilivyopangwa awali, kulingana na afisa wa Ikulu ya White House.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema Marekani inatarajia kujadili masuala kadhaa zaidi ya suala la nyuklia, ikiwa ni pamoja na majadiliano kuhusu makombora ya Iran, usaidizi wa mitandao ya wakala katika eneo lote na jinsi utawala wa Tehran unavyowatendea raia wa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *