
Haya ni baada ya mazungumzo huko Abu Dhabi kati ya Kamanda wa vikosi vya jeshi la Marekani Ulaya Alexus Grynkewich na maafisa waandamizi wa jeshi la Urusi na Ukraine.
Hatua hii inaweza kuashiria kusawazishwa kwabaadhi ya mahusiano kati ya Marekani na Urusi. Katika taarifa yake, jeshi la Marekani limesema lengo la kuanzisha tena mazungumzo hayo ni kuzuia kutoelewana na kuzidisha migogoro baina yao.
Marekani ilikuwa imesitisha mawasiliano kati ya jeshi lake na la Urusi muda mfupi kabla Urusi kuivamia Ukraine.
Vita hivyo vilivyoanza mwaka 2022, ndivyo vibaya zaidi kuwahi kufanyika Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia na pia ndiyo makabiliano makubwa zaidi kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi tangu wakati wa Vita Baridi.