Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Qatar,kama sehemu ya ziara yake nzima ya eneo la Ghuba ambayo ni ya kwanza tangu aingie madarakani, Merz hakuujibu moja kwa moja ukosoaji wa Abbas Araghchi kuhusu uongozi wa Ujerumani, ila ameitaka jamhuri hiyo ya Kiislamu iwe na nia ya suluhu kupatikana inapoingia katika mazungumzo na Marekani.

“Ningependa kuchukua fursa hii pia kutoa mwito kwa uongozi wa Iran kushiriki kikamilifu katika mazungumzo, kusitisha uchokozi wake, kusitisha mpango wake wa nyuklia kama ilivyokubaliwa kimataifa na zaidi ya yote, kuacha kuzitishia kijeshi nchi kama Qatar, Jordan na Israel,” alisema Merz.

Matamshi haya ya Merz yanatolewa wakati ambapo Iranimesema kuwa Araghchi pamoja na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff watashiriki mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran, huko Muscat, Oman hapo Ijumaa. Wawakilishi wa Oman ndio watakaokuwa wapatanishi katika mazungumzo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *