Katibu wa Kamati ya Uhusiano na Uenezi wa Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), Mess Chengula, amesema mpango wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wa kuuza sehemu ya akiba ya dhahabu ni hatua inayolenga kuimarisha uthabiti wa uchumi wa nchi, akisisitiza kuwa pia utasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni, hususan dola za Marekani.
Chengula ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema uamuzi wa Serikali kuuza sehemu ya dhahabu hiyo hautaleta athari yoyote hasi kwa sekta ya madini, kwani migodi bado inaendelea kuzalisha dhahabu kwa kiwango kikubwa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi