Kutumia tiba ya sumu iliyotengenezwa kwa ajili ya aina tofauti ya nyoka, inadhoofisha matibabu yake, alieleza.
Tatizo la bara zima
Kugongwa na nyoka bado ni tatizo kubwa lakini hakuna taarifa za kutosha Kusini mwa Jangwa la Sahara. Inakadiriwa kuwa watu hadi milioni moja wanagongwa na nyoka kila mwaka katika eneo hilo, huku vifo kati ya 7,000 na 20,000 vikiripotiwa kila mwaka. Kuna changamoto ya kuthibitisha takwimu hizi kutoka na mifumo dhaifu ya kutoa taarifa na matukio ambayo hayafikishwi hospitalini.
Afrika Magharibi pekee, vifo vinavyotokana na kugongwa na nyoka vinakadiriwa kuwa kati ya 3,500 na 5,400 kila mwaka. Katika hospitali moja nchini Nigeria, watu 6,687 waliogongwa na nyoka katika kipindi cha miaka mitatu pekee. Nchini Burkina Faso, kumekuwa na takwimu za watu 114,126 waliogongwa na nyoka katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano (2010–2014), kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Balla anaonya kuwa fikra za kwamba watu wanagongwa na nyoka katika maeneo ya vijijini pekee zinaweza kupotosha.
“Kama tulivyoona tukio baya la Ifunanya, nyoka wanaweza kuingia katika nyumba za mijini,” amesema. “Nyumba nyingi za mijini wakati fulani zilikuwa katika maeneo ya misitu. Wakati sehemu zao za kuishi zikiharibiwa au kubadilishwa, nyoka wanaondolewa katika maeneo hayo na kuchanganyana na binadamu. Mabustani ya maua na idadi kubwa ya panya mijini yanavutia nyoka.”
WHO imekuwa ikionya kuwa kugongwa na nyoka hakutakiwi kuonekana kama tatizo la afya ambalo halitakiwa kushughulikiwa.
Kwa raia wengi wa Nigeria, kifo cha Ifunanya kimefanya tuwe na mtazamo tofauti kuwa kugongwa na nyoka sio tatizo la vijijini pekee na kudhihirisha ukosefu wa utayari wa kukabiliana na hali ya dharura.