Karibu miaka kumi na tano baada ya kifo cha Muammar Gaddafi, aliyeuawa huko Sirte mnamo mwaka 2011, kuuawa kwa mwanawe Saif al-Islam siku ya Jumanne, Februari 2, huko Zintan, kaskazini magharibi mwa Libya, kunasikika kama mwisho unaowezekana wa ukoo wa Gaddafi madarakani nchini Libya. Mrithi wa mwisho wa kisiasa, ambaye alikuwa amebaki (Saif al-Islam), kwa makabila ya Libya na—hasa kwa ukoo wake—ishara ya kurejea kwa Gaddafi madarakani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Saif al-Islam Gaddafi hakika kitakuwa na matokeo kwa mustakabali wa mchakato wa kisiasa nchini Libya. Hakuna mwanachama mwingine wa ukoo huo anayefurahia umaarufu au ushawishi wake kwa sasa.

Kulingana na waangalizi kadhaa, “mauaji haya yanaweza pia kuwa na athari kwa pande pinzani nchini Libya.” Kutoweka kwa mtu anayeonekana kuwa na uwezo wa kuunganisha nchi “hakutakuwa kwa maslahi ya nchi,” kulingana na vyanzo hivyo.

Kwa Virginie Colombier, mtaalamu wa masuala ya sayansi ya siasa na profesa katika Chuo Kikuu cha Luiss Guido Carli huko Roma, kifo cha Saif al-Islam kinawanufaisha wadau kadhaa wa kisiasa waliomchukulia kama mpinzani.

Saif al-Islam Gaddafi alikuwa akiendeleza urithi wa Libya iliyoungana, Libya ilikusanyika karibu na mradi mkubwa wa maridhiano ya kitaifa. Hili halikupokelewa vyema na vituo viwili vikuu vya madaraka, ambao waliona matarajio ya mtu wa tatu kama tishio linalowezekana kwa uwezo wao wa kufikia makubaliano na kushiriki kile wanachopata kupitiamadaraka na rasilimali”, anasema Virginie Colombier, mtaalamu wa asuala ya sayansi ya siasa na Profesa katika Chuo Kikuu cha Luiss Guido Carli huko Roma

Maridhiano ya kitaifa, mwathirika wa kwanza

Maridhiano ya kitaifa ya Libya yanaonekana kuwa mwathirika wa kwanza wa mauaji ya Saif al-Islam. Kuwaleta Walibya pamoja katika mazungumzo kumeonekana kuwa haiwezekani. Si chini ya wajumbe saba maalum wa Umoja wa Mataifa wameshindwa hadi sasa, wakishutumu ukosefu wa nia kwa pande tawala kushiriki katika maridhiano haya.

Hii ilikuwa hivyo, kwa mfano, mnamo mwaka 2019 wakati utawala wa Marekani ulipompa Marshal Khalifa Haftar ruhusa ya kushambulia Tripoli, siku kumi kabla ya tarehe iliyopangwa. Mfuatano huu wa matukio ulisababisha kujiuzulu kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ghassan Salamé.

Mchakato dhaifu wa kisiasa

Saif al-Islam ndiye mtu wa tatu wa cheo cha juu aliyeuawa katika miezi ya hivi karibuni. Ongezeko hili la “mauaji ya kisiasa” linawatia wasiwasi wataalamu, ambao wanahofia kuyumba kwa usawa wa ndani wa nchi na changamoto kwa mchakato unaoendelea wa kisiasa.

Mauaji yake pia yanakuja wakati mgumu, kwani Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kuanzisha tena mazungumzo mapya ya kitaifa, mnamo mwezi Novemba mwaka huu.

Juhudi hizi zinaweza, tena, kushindwa. “Hatari sasa ni kwamba mchakato huu wa mazungumzo utavurugwa vibaya,” mtaalamu wa masuala ya Libya Virginie Colombier ameonya kwenye kituo chetu cha habari. Katika muktadha huu, kuibuka tena kwa mvutano hakuwezi kupuuzwa.

Hatimaye, wadau wa kikanda na kimataifa wanaweza kunufaika na kifo cha Saif al-Islam Gaddafi. Mara nyingi alionyesha kutokubaliana kwake na usimamizi wa sasa wa Libya, ambao aliuona kuwa umeathiriwa sana na mataifa ya kigeni, haswa Marekani na Uturuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *