Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani na kufanya shughuli za maendeleo bila kuangalia tofauti ya vyama vyao.

Akizungumza kwenye sherehe za Maulid yaliofanyika katika viwanja vya Madrasasatul Jumuiyyatul Islamiya wilayani Pangani mkoani Tanga na kusema kuwa suala la amani ni muhimu na ndio sababu ya watu kufanyakazi zao bila tatizo.

Ameongeza kuwa sherehe za Maulid ni fursa muhimu kwa Waumini wa Kiislamu kuendelea kuimarisha mshikamano, upendo na maadili mema katika jamii, huku akisisitiza umuhimu wa kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuilinda nchi dhidi ya migogoro na kuitunuku baraka ya amani na maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Sheikh Rajabu Abdallah wa Madrasasatul Jumuiyyatul Islamiya ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia maendeleo.

#StartvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *