Merz ameanza ziara yake ya siku tatu katika eneo la Ghuba.

Kabla ya kuondoka Ujerumani Kansela Merz alisema kuwa Ujerumaniinatafuta ushirikiano wa karibu katika eneo la Ghuba ili kuilinda nafasi yake katika mfumo wa dunia unaobadilika kwa haraka.

Merz amesema Ujerumani inataka kutanua mazungumzo yakena mataifa ya Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu katika eneo tajiri na la umuhimu wa kimkakati la Ghuba, ili kuimarisha usalama wake wa muda mrefu, mahusiano yake ya kiuchumi na usambazaji wa bidhaa, ikiwemo mafuta na gesi.

Hata hivyo, Kansela huyo aliyepokewa kwa heshima ya kijeshi alipowasili Riyadh, amekiri kuwa Ujerumani na mataifa hayo ya Ghuba hayawiani kimaadili na kimaslahi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *