Maeneo mawili zaidi katika jimbo la Darfur Kaskazini ya Um Baru na Kernoi sasa yameingia katika baa la njaa kufuatia utapiamlo wa kupindukia au unyafuzi kuvuka wiwango vya kutokuwa na uhakika wa chakula kwa mujibu wa tahadhari iliyotolewa leo na mfumo wa Umoja wa Mataifa wa tathimini ya uhakika wa chakula IPC. Tahadhari hiyo inaonesha kuwa zaidi ya nusu ya watoto katika baadhi ya maeneo Sudan wanakabiliwa na unyafuzi, hali inayohusishwa na mzozo unaoendelea, ufurushwaji mkubwa wa watu, uhaba wa chakula na upatikanaji mdogo wa misaada. Thahadhari hiyo ya IPC inaonya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi katika maeneo mengi yasiyofikika, ikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kufunguliwa kwa njia salama za misaada ili kuokoa maisha, hasa ya watoto.

media:entermedia_image:cc14f8ae-9b15-4d03-b6c1-55f15f918a45

Msaada wa UNIDS waendelea kurefusha maisha ya watu wanaoishi na VVU

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limekaribisha kwa dhati hatua ya Marekani kutia saini kuwa sheria kifurushi cha matumizi ya kimataifa chenye thamani ya dola bilioni 5.88, kwa ajili ya hatua za kimataifa za kukabiliana na virusi vya ukimwi VVU .

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametia saini kifurushi hicho tarehe 3 Februari 2026, ambacho kinatenga dola bilioni 4.6 kwa ajili ya msaada wa VVU kupitia Mkakati wa Afya ya Kimataifa wa America First, dola  bilioni 1.25 kwa Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria Global Fund, na dola milioni 45 kwa UNAIDS.

Ofisi ya UNRWA huko Gaza.

Ziad Abu Khousa

Ofisi ya UNRWA huko Gaza.

Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA  Phillippe Lazzarini amesema taarifa potofu dhidi ya UNRWA zinaendelea kulenga shirika hilo katikati ya mgogoro Gaza ikiwemo madai ya hivi karibuni kabisa, yaliyoibuliwa na video ya jeshi la Israel ikionesha mifuko mitupu ya unga karibu na mabomu, ambapo amesema ni taarifa za uongo na  hazijadhibitishwa. Ameeleza kuwa misaada ya kimataifa Gaza inaendelea kwa miaka, na mara chakula kinapogawiwa, mifuko hupakiwa tena na familia kwa matumizi mengine kutokana na uhaba mkubwa. Mwaka 2024 pekee, UNRWA ilisambaza karibu mifuko milioni 3 ya unga wa kilo 25, ambayo sasa ipo sehemu zote Gaza. UNRWA inasisitiza kuwa inaendelea kusaidia wakimbizi wa Palestina licha ya mashambulizi dhidi ya sifa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *