
Haya ni kulingana na ndugu wa al-Islam aliyeuwawa kwa kupigwa risasi juzi Jumanne katika mji wa kaskazini magharibi wa Zintan.
Kaka zake wawili wamesema al-Islam atazikwa katika mji wa Bani Walid ulioko kilomita 175 kusini mwa Tripoli.
Kila mwaka mji huo ulio na wakaazi karibu100,000 huadhimisha kuingia madarakani kwa Muammar Gaddafi kupitia mapinduzi yaliyofanyika mwaka 1969, kwa kuandamana barabarani wakiwa wamebeba picha za kiongozi huyo wa zamani.
Chini ya utawala wa miaka 40 wa baba yake, Seif al-Islam alionekana kama mrithi wake.
Alitangaza kuwania urais mwaka 2021 ila uchaguzi nchini humo uliahirishwa kwa muda usiojulikana.