PAMBA JIJI vs COASTAL UNION: Kocha wa Pamba Jiji Francis Baraza amesema maandalizi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union yamekamilika.

Kocha huyo amesema anatarajia wachezaji kuonesha kile alichowaelekeza ili waweze kupata alama tatu muhimu.

Naye mchezaji wa klabu hiyo Hassan Kibailo amesema wanajua jinsi msimamo ulivyo mgumu hivyo watapambana kupata alama kujiweka katika nafasi nzuri.

Ni mechi ya NBC Premier League ambayo itapigwa saa 8:00 mchana LIVE #Azam Sports1HD.

#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *