Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amemwambia mwenzake wa China, Xi Jinping, kwamba Urusi itawajibika ipasavyo huku mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani ukiwa unamalizika Februari 5.
Walizungumza kwa njia ya video kabla ya kuanza kwa mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kichina, Februari 4.
Msaidizi wa rais wa Urusi, Yury Ushakov, amesema Mkataba wa Kupunguza Silaha za Kimkakati, au New START, ulikuwa kwenye ajenda ya viongozi hao.
Alimnukuu Putin akisema Urusi itatenda “kwa njia iliyopimwa na yenye uwajibikaji kulingana na uchambuzi wa kina wa hali ya usalama kwa ujumla” na kwamba nchi hiyo “inaendelea kuwa tayari kutafuta njia za mazungumzo ili kuhakikisha uthabiti wa kimkakati.”
Katika mazungumzo hayo, Xi alimwalika Putin kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa kongamano la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki, APEC ambao China itakuwa mwenyekiti mwezi Novemba.
Ushakov alisema Putin “kwa hakika” atakuwa tayari kuhudhuria mkutano huo.