Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi na ujumbe wake, amerejea tena jijini Washington nchini Marekani, miezi miwili baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani na Rwanda, ambapo unaonekana kutotekelezwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje Marco Rubio na  Kamati ya Senate ya Marekani inayoshughulikia mambo ya nje, kujadili hali ya usalama Mashariki mwa DRC na utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Washington uliotiwa saini mwaka uliopita.

Maseneta hao  wakiongozwa na Chris Smith,  anayeongoza kamati inayoshughulikia maswala ya Afrika, wameishtumu Rwanda kwa kutotekeleza mkataba huo kikamilifu, kufuatia waasi wa M23/AFC inaowaunga mkono kuendelea kudhibiti maeneo mbalimbali mashariki mwa DRC licha ya kutakuwa kuondoka, na sasa wanataka viongozi wa Kigali kuwekewa vikwazo.

Ziara hiii inakuja wakati huu wafuatiliaji wa mkataba huo wa Washington wakisema hakuna hatua iliyopigwa, kwenye utekelezwaji wake, kinyume na ilivyotarajiwa.

Miongoni mwa changamoto zinazoelezwa kusababisha kutotekelezwa kwa mkataba huo ni kuendelea kwa machafuko, kushindwa kuwatokomeza waasi wa FDLR wanaotishia usalama wa Rwanda na changamoto za waathiriwa wa vita kutopata misaada ya kibinadamu kama chakula na dawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *