Watu wanne, wakiwemo raia wawili wa China, wameshtakiwa leo Alhamisi, Februari 5, kufuatia kukamatwa kwao kusini-magharibi mwa Ufaransa. Wanashukiwa kujaribu kusambaza taarifa za kijeshi kwa mamlaka ya China.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa kwao kuliwezekana kwa sababu wapelelezi wanaodaiwa hawakuwa waangalifu sana. Walichagua mji mdogo wenye wakazi zaidi ya 3,000 kusini mwa Bordeaux ili kukodisha nyumba kupitia Airbnb. Katika bustani, waliweka sahani kubwa ya setilaiti, yenye kipenyo cha takriban mita mbili. Usakinishaji wake uliweza kuonekana kwa urahisi. 

Mnamo Januari 31, polisi wa Ufaransa waliarifiwa, na uchunguzi ukakabidhiwa kwa DGSI, Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Ndani. Siku iliyofuata, maafisa waligundua mfumo wa kompyuta uliounganishwa na sahani za setilaiti. Uliundwa ili kukamata data ya setilaiti kutoka kwa mtandao wa Starlink, mtambo unaotoa huduma ya intaneti ya setilaiti ya SpaceX, kampuni iliyoanzishwa na Elon Musk.

Raia wa China wanatafuta taarifa za kijasusi za kijeshi

Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka, kifaa hicho kilikusudiwa kunasa mawasiliano kati ya “vyombo muhimu vya kijeshi.” Mamlaka ya Ufaransa inawashuku kufanya kazi kwa niaba ya Beijing.

Raia hao wawili wa China, wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini, wamekuwa Ufaransa kwa visa vya kazi. Walisema ni wahandisi wa kampuni ya vifaa vya mawasiliano visivyotumia waya. Watu wengine wawili waliokamatwa, wenye umri wa miaka 39 na 45, ambao uraia wao haujatajwa, wanashukiwa kutoa msaada wa vifaa kwa watu hao wanashukiwa kuwa majasusiwa China.

Ufaransa, inalengwa kwa idra ya ujasusi ya China

Hii sio kesi ya kwanza ya ujasusi wa China kuzuka nchini Ufaransa. Mnamo mwaka 2021, ripoti ya INSERM, Taasisi ya Ufaransa ya Utafiti wa Mikakati katika Chuo cha Kijeshi, kuhusu shughuli za China duniani kote, ilionyesha kwamba Ufaransa ilikuwa kipaumbele kwa idara ya ujasusi za Beijing.

Tangu wakati huo, kesi zimeongezeka, ikiwa ni pamoja na tukio lingine mnamo mwaka 2025 la kupelekwa kwa antena haramu karibu na Toulouse. Kesi hiyo ilifichuliwa na Intelligence Online, chombo cha habari kilichojitolea kwa ujasusi na masuala ya kidiplomasia. “Kulikuwa na wasiwasi kwamba taarifa zilizonaswa zingeweza kusababisha uharibifu wa setilaiti, iliyotolewa na Ufaransa kwa nchi ya tatu,” anaelezea Jérémy André, mwandishi mkuu wa habari wa Intelligence Online. “Haya ni mambo halisi sana. Huu si uchunguzi wa kawaida. Leo, kuna vita vya siri, na vinaendeshwa, hasa, angani.”

Katikati ya mwezi Desemba, profesa katika Taasisi ya Uhandisi na Mekaniki ya Bordeaux alishtakiwa kwa “kushirikiana na nchi ya kigeni.” Anashutumiwa kwa kuruhusu ujumbe wa China katika maeneo yaliyopigwa marfuku kuingia na nyeti.

Kusini Magharibi mwa Ufaransa: Eneo nyeti

Kesi nyingi za hivi karibuni za ujasusi wa Kichina zimetokea kusini magharibi mwa Ufaransa, kati ya Bordeaux na Toulouse, kitovu cha tasnia ya anga ya Ufaransa na viwanda vinavyohusiana na jeshi.

Katika kesi ya hivi karibuni ya sahani ya setilaiti iliyosambazwa kusini mwa Bordeaux, kijiji kilichochaguliwa, Camblanes-et-Meynac, kiko kilomita chache tu kutoka kituo pekee cha ardhini cha Starlink nchini Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *