
Hii ni baada ya wanamgambo wa RSF kuuteka mji mkuu El-Fasher na kusababisha idadi kubwa ya watu kuyakimbia makaazi yao.
Haya yamesemwa na wataalam wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Katika tahadhari iliyotolewa na Shirika la KutathminiUsalama wa Upatikanaji wa Chakula Duniani, IPC, wataalam wa chakula wamesema hali katika maeneo ya Um Baru na Kernoi karibu na mpaka wa Chad sasa imeshavuka kiwango cha utapiamlo.
Haya yanafanyika wakati ambapo Uingereza imewawekea vikwazo vipya watu sita wanaoshukiwa kufanya ukatili katika vita vya Sudan au kuchochea vita hivyo kwa kupeleka vifaa vya kijeshi au mamluki nchini humo.
Vikwazo hivyo vinawalenga makamanda wakuu wa wanamgambo wa RSF ambao wapiganaji wake wanashukiwa kuwauwa raia na kutumia ubakaji kama silaha ya vita.
Miongoni mwao ni kamanda wa RSF Hussein Barsham, Abu Aqla na Mohamed Kaikal.