Haya yanafanyika wakati ambapo mpatanishi wa Marekani Steve Witkoff amekiri kuwa kuna “kazi” kubwa mbele yao katika harakati za kutaka kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Witkoff ameandika katika mtandao wa kijamii akithibitisha kuachiwa kwa wafungwa hao na baadae wizara ya ulinzi ya Urusi nayo ikathibitisha kuwa pande hizo mbili zimebadilishana wafungwa 157 kila mmoja.

Huku mazungumzo yakiwa yanaendelea huko Abu Dhabi, sehemu kubwa za mji mkuu wa Ukraine bado hazina huduma za umeme katika kipindi cha baridi kali, baada ya mashambulizi ya mfululizo ya Urusi kukata mfumo wa usambazaji wa umeme katika nyumba kadhaa za makaazi mjini Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *