Mazungumzo hayo yanalenga kuvimaliza vita vya Ukraine vilivyoanza kufuatia uvamizi wa Urusi mwaka 2022.

Mazungumzo hayo ndiyo ya hivi karibuni katika juhudi za kidiplomasia za kusitisha vita hivyo vilivyosababisha mamilioni kuyakimbia makaazi yao, huku maeneo mengi ya Ukraine mashariki na kusini yakiwa yameharibiwa vibaya.

Haya yanafanyika wakati ambapo mjumbe wa Rais Vladimir Putin, Kirill Dmitriev akisema leo kuwa kuna hatu zimepigwa katika kupata makubaliano ya amani.

“Ishara moja ni kuwa wachochezi wa vita kutoka Ulaya, kutoka Uingereza wanajaribu kila mara kuzuia kupigwa kwa hatua, wanajaribu kuingilia kati kila mara. Na kadri majaribio hayo yanavyozidi, ndivyo tunavyoona kwamba kuna hatua zinazopigwa, mambo yanasonga mbele katika mkondo mzuri,” alisema Dmitriev.

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa wanajeshi 55,000 wa Ukraine wameuwawa tangu Urusi ianze uvamizi wake nchini humo miaka minne iliyopita. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha Ufaransa, Zelensky amesema sehemu kubwa ya wanajeshi hao hawajulikani walipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *