Ujenzi wa takienta unatumia nyenzo za kiikolojia zinazopatikana ndani eneo lao, ikiwa ni pamoja na udongo, mbao, matunda ya shea, majani, mmea wa haibiskasi, mitende, mtama na samadi ya ng’ombe. Ubunifu na utumiaji wa nyenzo hizi pia huleta mazingira bora ya hali ya hewa ya asili.

Zikiwa nane zinaitwa sikien.

Taratibu za kipekee za ujenzi wa Batammariba zinaonyesha heshima kubwa ya jumuiya na uhusiano wake na ardhi.

Ujenzi wa takienta unapofanyika, kunakuwa na mgawanyiko wa matumizi,  moja inaweza kutumika kama sehemu ya kupikia, nyingine kama vyumba vya kulala, na nyingine kama hifadhi ya chakula na mifugo.

Katika ghorofa ya kwanza ya takienta unaweza pata jiwe la kusagia chakula, jiko, ng’ombe, sehemu ya kufanyia ibada, chumba cha mzee na kwenye ghorofa nyingine ambapo unakuta dari, vyoo na vyumba vya kulala.

Wanaamini kuwa ghorofa ya kwanza ni mahali pa watu kuishi wakati ghorofa ya pili imehifadhiwa kwa roho ya mababu wao ambao wanaamini bado wanawalinda.

Paa za nyasi kawaida zinakwua juu ya takienta,  na hutumika ili kuleta hali ya baridi wakati wa kiangazi.

Mlango mkuu wa kila takienta lazima unawekwa kwa mujibu wa hatua ambayo jua huvuka upeo wa macho wakati wa machweo na kwenye majira ya baridi.

Jamii nzima inahusika katika ujenzi wa takienta, huku wanaume wakiwa majukumu la kuinua kuta na wanawake kuandaa, kupaka na kupamba plasta ya udongo inayozifunika nyumba.

Hata hivyo,  wanawake peke yao wanawajibika kwa matengenezo ya kila mwaka ya takienta, ikiwemo pamoja na kukarabati kuta za zamani.

UNESCO ilizitambua nyumba hizo mwaka 2003 kama eneo la Urithi wa Dunia na kuziita “mazingira ya utamaduni hai.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *