
Wataalamu walioagizwa na Umoja wa Mataifa wameonya mnamo Februari 5, 2025, kwamba njaa inatishia kuenea katika maeneo mawili mapya magharibi mwa Sudan, kufuatia El-Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, kuanguka mikononi mwa waasi wa RSF, hali ambayo imewalazimu watu wenye njaa kwenda maeneo jirani ambayo tayari ni dhaifu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
El-Fasher ilikuwa ngome ya mwisho ya jeshi huko Darfur, ambayo ilianguka mikononi mwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) mwishoni mwa mwezi Oktoba.
“Vizingiti vya utapiamlo mkali vimezidi” katika miji ya Umm Barou na Kernoi, karibu na mpaka wa Chad, kulingana na wataalamu kutoka Uainishaji Jumuishi wa Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC), shirika lililoagizwa na Umoja wa Mataifa lenye makao yake Roma.
Katika mji wa Oum Barou, 18.1% ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo mkali mkali. Katika mji wa Kernoi, kiwango kimefikia 7.8%. Wataalamu wanahusisha hali hii na “wimbi kubwa” la raia kufuatia kuanguka mikononi mwa waasi kwa El-Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi huko Darfur, ambalo lilipoteza mji huo mwishoni mwa mwezi Oktoba kwa kwa faida ya Vikosi yva Msaada wa Haraka (RSF).
“Mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani”
Mashambulizi ya RSF, yaliyojaa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, yamewatimua watu zaidi ya 127,000, kulingana na Umoja wa Mataifa, na kuzidisha shinikizo kwa “rasilimali na uwezo wa jamii za wenyeji,” wataalam wanasema.
Vita hatari kati ya jeshi na Vikosi vya RSF vimeikumba Sudan tangu mwezi Aprili 2023. Karibu miaka mitatu ya migogoro imesababisha makumi ya maelfu ya watu kuuawa, kuwafanya watu wapatao milioni 11 kuhama makazi yao, na kusababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.
Zaidi ya watu milioni 21 sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, na theluthi mbili ya idadi ya watu wanahitaji msaada wa dharura. Umoja wa Mataifa umeonya kwamba akiba yao ya chakula inaweza kuisha ifikapo mwisho wa mwezi Machi.