
Wachambuzi wanasema muda aliochagua Xi kufanya mazungumzo na viongozi hao wawili ni muhimu wakati ambapo Beijing inajiweka katika nafasi ya kuwa nchi imara yenye nguvu duniani.
Kulingana na Rais Trump, mazungumzo yake na Xi yalijikita katika biashara, vita vya Urusi nchini Ukraine na kuhusu Iran. Xi lakini ametoa tahadhari kwa Marekani kuwa makini katika kuiuzia Taiwan silaha.
Taiwan ni kisiwa kinachojitawala ila China inadai ni sehemu ya himaya yake na imeapa kukichukua kisiwa hicho kwa nguvu iwapo itahitajika.
Na saa chache baadae katika mazungumzo yake na Putin, viongozi hao wawili walizungumza kwa saa moja na nusu wakisifu kuimarishwa kwa mahusiano ya nchi zao wakati wanapojaribu kuungana dhidi ya nchi za Magharibi.