Aliyekuwa Msaidizi wa Karibu wa Rais, Balozi Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziiri ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa balozi alikuwa msaidizi wa karibu wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu kuingia madarakani baada ya kifo cha Rais John Magufuli.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bakari Machumu imesema kuwa Waziri anachukua nafasi ya Dkt Hashil Twahin Abdallah atakayepangiwa kazi nyingine.

#starTvupdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *