Araghchi, ameiambia televisheni ya taifa ya Iran IRNA kwamba katika mazingira hayo, walibadilishana maoni na kuongeza kuwa pande hizo mbili zitaamua kuhusu mipangilio na wakati wa mazungumzo mengine katika tarahe ya baadaye.

Mwanadiplomasia huyo pia amesema mazungumzo hayo na Marekani yalikuwa “mwanzo mzuri sana” lakini kwamba wanaoshiriki mazungumzo hayo sasa wanapaswa kuzungumza na viongozi wao.

Ameongeza kuwa mazungumzo hayo yanafanyika katika awamu nyingi na kwamba lengo lao kuu ni kutafuta mfumo wa mazungumzo zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *