ASKOFU Mkuu wa Global Concert Church (NGURUMO YA UPAKO), Nabii Mkuu na Mstahiki Meya wa Amani Duniani, Profesa GeorDavie K. Moses, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuelekea kutimia kwa siku 100 tangu aapishwe kushika wadhifa huo.
Akizungumza kuhusu uongozi wa Rais Dk. Samia, Profesa Moses amesema kuwa katika kipindi kifupi, Rais Dk. Samia ameweza kuleta uchangamfu na matumaini mapya kwa wananchi, hususan kupitia miradi inayolenga kuwawezesha wanawake, Vijana na Makundi Maalumu kiuchumi.
Ameeleza kuwa hatua za awali zilizochukuliwa na Rais Dk. Samia zinaonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania, huku akibainisha kuwa kuanzishwa kwa miradi ya kinamama ni nyenzo muhimu ya kusaidia jamii kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Profesa GeorDavie ameipongeza Serikali kwa kuunda Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, akisema hatua hiyo ni ya busara na inaonesha utayari wa Rais Dk. Samia kusikiliza maoni ya wananchi na kushughulikia masuala nyeti kwa uwazi na haki.
“Rais Dk. Samia ameonyesha nuru mbele yetu, ameweka wazi maono yake kwa ajili ya Watanzania na kwa mtazamo wangu tunaelekea mahali pazuri,” amesema Profesa GeorDavie.
(Feed generated with FetchRSS)