Rais wa Rwanda Paul Kagame ameihimiza nchi yake kujitegemea zaidi, huku wito ukiongezeka nchini Marekani wa kuweka vikwazo zaidi kuhusu ushiriki wake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu wa Rwanda Kigali hapo jana, Kagame alionekana kujibu kwa kusisitiza uhuru wa nchi hiyo akisema tumejitolea kujitegemea ili uhai wetu usitegemee bahati, au nia njema ya wengine ambao wanaweza kuchagua kutusaidia leo na kujiondoa kesho.

Kagame aliongeza kusema katika kipande cha video iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya ofisi ya rais katika mtandao wa X kwamba kujitegemea ndio kipaumbele kikuu cha Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *