Hii leo, wizara hiyo ya mambo ya ndani ya Uingereza, ilitangaza hatua hiyo ya Kongo huku Mahmood akisema kwamba ujumbe wake uko wazi kuwa ikiwa nchi za kigeni zitakataa kuwakubali raia wake wanaorejea nyumbani, zitakabiliwa na athari.

Mahmood alitoa tishio hilo kwa Kongo mwishoni mwa Desemba mwaka jana kutokana na kukosekana kwa ushirikiano kuhusu wahalifu wa kigeni wanaorejea nchini mwao pamoja na wale wasiokuwa na vibali vya kuishi Uingereza.

Wakati huo huo, alisitisha kipaombele kwa wanadiplomasia wa Kongo na watu mashuhuri pamoja na kuharakisha utoaji wa haraka wa visa kwa raia wa nchi hiyo.

Kongo ni nchi ya tatu kufikia makubaliano na Uingereza baada ya kutishiwa kuwekewa vikwazo vya visa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *