KUTOKA KWA MADIBA: Timu ya Taifa ya Tanzania imepata ushindi katika michezo yake miwili iliyocheza leo Februari 6, 2025 kwa kuifunga Zimbabwe kwa fremu 14-11 na baadae ikawafunga wenyeji Afrika Kusini kwa fremu 13-12.

Ushindi dhidi ya Afrika kusini ni kisasi ambacho kimelipwa na Tanzania Wanaume ambao walipoteza katika mchezo wa fainali za mwaka 2023 ambapo Tanzania ilipoteza kwa fremu 11-13.

Baada ya kupata matokeo hayo sasa Tanzania inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi ambapo timu saba zinashiriki katika mashindano hayo ya All African Cue Championshipo yaliyoandaliwa na Chama cha Pool Afrika (AAPA).

Kwa upande wa wachezaji Binafsi (Single) Mtanzania Jackson Ng’anyi amepoteza nusu fainali mbele ya bingwa wa Afrika Kusini Harry Martin baada ya kufungwa kwa fremu 3-7.

Sasa anasubiri kucheza mchezo wa kumpata mshindi wa tatu dhidi ya Lutham Banda ambae amepoteza dhdi ya Shaun Martheze atakaecheza fainali Kesho Jumamosi.

Jumla ya washiriki 38 walishiriki katika kipengele hicho cha wachezaji binafsi.

#PoolTable

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *