Maafisa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania waliomaliza muda wao wa kuhudumu katika operesheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini wamevishwa nishani katika gwaride maalum, ikiwa ni kutambua mchango wao katika kudumisha amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi kinara katika kuchangia askari kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.
Askari waliovishwa nishani wamesema licha ya changamoto za mazingira magumu, waliendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutoa elimu ya amani kwa jamii.
Aidha, wamewashukuru majeshi wenzao kwa ushirikiano mzuri wakati wa misheni hiyo na kuwaomba wananchi wa Sudan Kusini kuendelea kulinda na kudumisha amani ya nchi yao.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi