Saif al-Islam, mwenye umri wa miaka 53, aliuawa siku ya Jumanne ndani ya nyumba yake katika mji wa Zintan, uliopo kilomita 136 (maili 85) kusini-magharibi mwa Tripoli, kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Libya.

Mamlaka zilisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa alipigwa risasi hadi kufa, lakini hazikutoa maelezo zaidi.

Wanachama wa kisiasa ya Saif al-Islam baadaye walitoa taarifa kuwa “watu wanne waliovaa barakoa” waliivamia nyumba yake na kumuua, wakiyataja kuwa “mauaji ya kikatili na ya hila,” baada ya kuzima kamera za usalama.

“Maumivu ya kumpoteza yananilemea sana moyoni, na yanaongezeka zaidi kwa sababu siwezi kumuaga nikiwa ndani ya nchi yangu — maumivu ambayo maneno hayawezi kuyapunguza,” aliandika kaka yake Saif al-Islam, Mohamed Gaddafi, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook siku ya Ijumaa.

“Lakini faraja yangu ni kwamba wanaanchi waaminifu wa taifa wanatimiza wajibu wao na watampa buriani inayostahili hadhi yake,” aliandika kaka huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *