Mbunge wa viti maalumu mkoa wa njombe kwa Tiketi ya CCM Rebecca Sanga Nsemwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bunge Sports Club.
Rebeca amepata kura 158 dhidi ya mshindani wake Mh.Abbas Tarimba Mbunge wa jimbo la Kinondoni ambaye amepata kura 41.
Bunge Sports Club ni taasisi inayohusika na kukuza michezo na burudani miongoni mwa wabunge na watumishi wa bunge.
Nsemwa ameahidi kuwa chachu ya kukuza michezo nchini kupitia nafasi hiyo aliyochaguliwa na wabunge na kwamba ni matarajio yake kuona wabunge wanafika mbali katika michezo hiyo inayoshirikisha Nchi Saba za Afrika Mashariki.
Aidha katika uchaguzi huo Mh.Thomas Kampala amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti huku Mh.Festo Sanga akichaguliwa kuwa
Meneja wa Timu,na kwamba majukumu yatatekelezwa kwa pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ambao ni Mhe. Saashisha mafuwe,Mhe.Zulfa Omar,Mh Agnes Marwa,Mhe. Chistina Mzava na Mhe. Dickson Lutevele.
#RFAOnline
#Habaristartv
@dkhan1410