MTIBWA vs NAMUNGO FC: Kocha wa Mtibwa Sugar, Yusuf Chipo amesema wataanza kwa kuangalia mapungufu ya mpinzani wao yalipo ili wakifanya mabadiliko ya wachezaji yakatoe matokeo chanya uwanjani.
Naye nahodha wa kikosi hicho, Haroun Lyawatwa amesema wachezaji wana morali na wamejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo, hivyo watacheza kwa tahadhari kuzitafuta alama tatu ili waendelee kubaki katika nafasi nzuri.
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates