Shirika hilo limesema shambulizi hilo limetokea katika kituo cha afya kilichoko kwenye mji wa Walgak na kusababisha kusitishwa kwa huduma muhimu kwa mamia ya watoto na familia zao.

 Save the Children imethibitisha kwamba hakuna mfanyakazi wake yeyeote aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo la Sudan Kusini, lakini linasitisha shughuli zake kwenye eneo hilo na kuwaondoa wafanyakazi wake.

Chris Nyamandi, Mkurugenzi wa Save the Children Sudan Kusini, amesema ikiwa vituo vya misaada vinashambuliwa, ni raia, hasa watoto ndiyo wanaathirika zaidi. Nyamandi amesema vitendo hivyo havikubaliki na lazima vikomeshwe.

 Shambulizi hilo limetokea jana Alhamisi, baada ya hospitali ya Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, kuharibiwa kwa shambulizi la anga huko Lankein siku ya Jumanne na kuharibu ghala lake kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *