Rais wa Jamuhuri ya Uganda, Yoweri Museveni anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku moja ya kikazi.
Rais Museveni atawasili keaho Jumamosi Januari 7,2026 na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan.
Taarifa ya Ikulu inasema kuwa mazungumzo hayo yatajikita kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ushirikiano wakiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, miongoni mwa mambo yatakayozungimziwa ni suala la nishati hususani Mradi wa Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP), unaotarajiwa kuleta manufaa kwa nchi zote mbili na kanda.
#StarTvUpdate