
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameahidi ushirikiano wa karibu zaidi wa ulinzi na washirika muhimu katika eneo la Ghuba, akisema ni kwa maslahi ya pande zote kwa sababu wanataka kuhakikisha kwamba dunia inakuwa salama zaidi.
Akizungumza akiwa katika ziara yake Qatar jana Alhamisi Merz alisema dunia itakuwa salama zaidi ikiwa tu tutajilinda pia.
Merz alisema wakati Ujerumani itakapotambua washirika wa kuaminika katika masuala ya ushirikiano kama vile Qatar na Saudi Arabia, nchi hizo zinaweza kutarajia ushirikiano mkubwa zaidi wa ulinzi kuliko miaka ya hivi karibuni.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba hii haimaanishi kwamba Ujerumani ingesambaza na ingesafirisha silaha nje bila usimamizi na udhibiti.