Mkuu wa shirika la Umoja Mataifa la haki za binadamu Volker Turk ameelezea kuwa baada ya wafadhili wakuu kujiondoa mwaka jana, ufuatiliaji wa haki za binadamu umo hatarinikutokana na ukosefu wa fedha ambazo zingesaidia kuwabainisha waathiriwa na pia wahusika katika suala zima la kulinda haki za binadamu.

Mwaka huu ofisi hiyo inahitaji dola milioni 400 kuendesha mipango yake katika nchi mbalimbali kando na zile za matumizi ya shughuli za kila siku kamavile mishahara kwa wafanyakazi wake.

Turk amelezea masikitiko yake kwamba hali hii ya uhaba wa fedha inatokea wakati ulimwengu ukikabiliwa na kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

 “Kuondolewa na kupunguzwa kwa misaada kunaifungua mikono ya wanaohusika katika ukiukaji wa haki za binadamu kufanya vile wapendavyo. Kushamiri kwa matukio hayo kunamaanisa mwaka huu wa 2026 tunahitaji kuongeza juhudi zaidi.”

USA New York 2025 | Donald Trump -Baraza Kuu la UN
Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano mkuu wa UNPicha: John Angelillo/UPI Photo/IMAGO

Athari za sera za Trump

Mwaka uliopita shirika hilo lilikuwa na bajeti ya dola milioni 500 lakini lilipokea dola milioni 258 tu. Hii ilitokana na hatua ya utawala wa rais Donald Trump kuacha kutoa misaada ya kifedha kwa ofisi hiyo.

Mwaka uliotangulia chini ya utawala wa rais Joe Biden, Marekani ilitoa mchango wa dola milioni 36. Ufaransa ambayo pia ni miongoni mwa wafadhili 113 ambao wamekuwa wakitegemewa na ofssi hawakutoa fedha zozote huku Uingereza ikipunguza mchango wake. Hata hivyo mataifa ya Uswisi, Ujerumani and Umoja wa Ulaya yalizidisha michango yao.

Kutokana na hali hii ya uhaba wa fedha kamishna mkuu Turk alilazimika kuchukua maamuzi ya kufunga ofisi kadhaa hasa nchini Colombia na pia kupunguza shughuli zao kwa asili mia 60 nchini Myanmar. Aidha walipunguza mipango yao ya kupigania haki za watu 600 walio vizuizini nchini Chad.

Vivyo hivyo shirika hilo la haki za binadamu limeshindwa kushugulikia hali nchini Ukraine na katika Mamlaka ya Palestina. Katika ripoti yake ofisi hiyo inaelezea kuwa imeweza kuwasaidia zaidi ya watu 67,000 walionusurika mateso na pia kutoka utumwa mamboleo. Aidha waliwea kuchunguza na kuandaa taarifa zaidi ya elfu kumi kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Siku ya Ijumaa Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba dunia inaelekea pabaya kutokana na ukosefu wa fedha za Umoja huo kuweza kutekeleza majukumu yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *