Idara ya Moto na Usimamizi wa Majanga nchini Japani inasema watu 42 wamefariki katika matukio yanayohusiana na hali mbaya za msimu wa baridi kali na theluji nyingi nchini humo tangu Januari 20.

Kufikia saa 2:30 asubuhi Februari 6, watu 15 walikuwa wamefariki mkoani Niigata, 8 mkoani Akita, 5 katika kila mkoa wa Aomori na Yamagata, na 4 mkoani Hokkaido. Mikoa ya Iwate, Fukui, Nagano, Kyoto na Shimane iliripoti kifo kimoja kila mkoa.

Jumla ya watu 444 wamepata majeraha makubwa au madogo.

Vifo vingi vilitokea katika ajali wakati wa kazi ya kuondoa theluji au kutokana na magonjwa ya ghafla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *