Watu wasiopungua 22 wakiwemo wahudumu 4 wa sekta ya afya wameuawa na wengine wawane kujeruhiwa baada ya wanangambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) jana kuishambulia hospitali ya jeshi ya al Kuweik katika jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetoa taarifa na kueleza kuwa wahanga wa hujuma ya wanagambo wa RSF  ni pamoja na Mkurugenzi wa Matibabu wa hospitali  ya kijeshi hiyo na wafanyakazi wengine watatu wa afya.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umelaani shambulio hilo na kusema kitendo cha kuvilenga kwa mashambulizi vituo vya afya na matibabu na watoa huduma ni sawa na jinai ya kivita na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu na mikataba inayohakikisha ulinzi wa raia na taasisi za matibabu.

Taarifa ya Mtandao wa Madaktari wa Sudan imeongeza kuwa shambulio la RSF katika hospitali ya jeshi ya al Kuweik huko Kordofan Kusini si tukio la kando, bali ni sehemu ya mashambulizi mtawalia ya wanamgambo hao huko Kordofan Kusini ambayo yamezipelekea hospitali kadhaa jimboni humo kusitisha huduma na hivyo kushadidisha mgogoro wa kibinadamu.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umesema kuwa wanamgambo wa RFS wanabeba dhima ya hujuma hiyo dhidi ya hospitali na kuitaka jamii ya kimataifa, mashirika ya Umojaj wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu kuchukau hatua haraka iwezekanavyo kukomesha mashambulizi dhidi ya hospitali na vituo vya afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *