Picha kutoka eneo hilo zilionyesha miili yenye damu ikiwa sakafuni ndani ya msikiti huo na kuzunguzwa na vipande vya vioo, uchafu na waumini waliokuwa na hofu.

Makumi ya wengine waliokuwa wamejeruhiwa walikuwa wamelala kwenye bustani ya msikiti huo wakati maafisa wa polisi walipokuwa wakitafuta usaidizi.

Mshambuliaji alizuiwa katika lango la msikiti

Maafisa wawili waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwa kutokuwa na idhini ya kuzungumza na waandishi wa habari, wanasema mshambuliaji huyo alisimamishwa kwenye lango la msikiti huo kabla ya kulipua bomu hilo.

Serikali kuzisaidia familia za waathiriwa

Baada ya kuwatembelea waliojeruhiwa hospitalini, waziri wa masuala ya bunge  wa Pakistan Tariq Fazal, alisema wanatoa msaada wote unaohitajika kwa familia za waliopoteza wapendwa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *