Marekani. Rapa wa Marekani, Asap Rocky, 37, amejibu kwa ustadi swali la mwanafunzi mdogo aliyeuliza kama tayari amefunga ndoa na mpenzi wake, Rihanna, 37, ambaye pia ni mama watoto wake.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika kipindi cha Celebrity Substitute ambacho huwapa wanafunzi wa shule za umma fursa ya kuwauliza maswali watu mashuhuri.
Katika kipindi hicho, mtoto mmoja alimuuliza Asap Rocky swali akitaka kufahamu kama yeye na Rihanna walishafunga ndoa. Hata hivyo, rapa huyo hakujibu moja kwa moja bali alichagua kutumia utani kukwepa swali hilo.
“Umeuliza swali la kuvutia,” alisema Rocky, kabla ya kumuuliza mtoto huyo kama angependa Rihanna ndio awepo katika kipindi hicho badala yake.
“Unamtaka Rihanna, huh? lakini umenipata mimi. Leo umenipata mimi,” aliongeza rapa huyo, mkali wa kibao cha Fashion Killa (2013).
Asap Rocky na Rihanna waliweka wazi uhusiano wao Novemba 2020. Kwa sasa, wawili hao wana watoto watatu, RZA, 3, Riot Rose, 2, na Rocki Irish mwenye umri wa miezi mitano.
Katika kipindi hicho hicho, Asap Rocky pia alizungumzia namna yeye na Rihanna wanavyowalea watoto wao katika mazingira yenye mchanganyiko mkubwa wa muziki.
“Ninawachezea watoto wangu aina zote za muziki, kuanzia nyimbo za zamani za Michael Jackson, na pia reggae. Tunaishi kwenye familia yenye muziki mwingi, kwa hiyo kuna mchanganyiko mkubwa,” ameeleza.
Mapema mwezi huu katika kipindi cha The Tonight Show Starring Jimmy Fallon, Asap Rocky pia alifunguka kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na nje ya klabu moja jijini New York wakati yeye bado hajawa maarufu.
“Yeye tayari alikuwa Rihanna. Mimi sikuweza hata kuingia ndani ya klabu,” alisema Asap Rocky na kuongeza.
“Walinzi hawakutaka kuniruhusu kuingia. Nilikuwa na rafiki zangu Virgil Abloh na Matthew Williams, tukawa tunabishana nao, ndipo yeye akatoka nje na tukatazamana macho kwa macho. Nilikuwa kama nipo kwenye mshangao,” alieleza.
Kwa sasa, Asap Rocky anaendelea kusherehekea mafanikio ya albamu yake ya nne, Don’t Be Dumb (2026) iliyotoka Januari 16 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200.
Mafanikio hayo yalimfanya Rihanna kujitokeza katika mitandao ya kijamii na kuonyesha yake furaha. “Nipo hapa kuwajulisha kuwa baba wa watoto wangu ana albamu namba moja…,” aliandika Rihanna kupitia ukurasa wake wa X, zamani Twitter.
Rapa wa Marekani, Asap Rocky, 37, amejibu kwa ustadi swali la mwanafunzi mdogo aliyeuliza kama tayari amefunga ndoa na mpenzi wake, Rihanna, 37, ambaye pia ni mama watoto wake.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika kipindi cha Celebrity Substitute ambacho huwapa wanafunzi wa shule za umma fursa ya kuwauliza maswali watu mashuhuri.
Katika kipindi hicho, mtoto mmoja alimuuliza Asap Rocky swali ikitaka kufahamu kama yeye na Rihanna walishafunga ndoa. Hata hivyo, rapa huyo hakujibu moja kwa moja bali alichagua kutumia utani kukwepa swali hilo.