#HABARI: Serikali ya Awamu ya Sita imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kulinda haki za wafanyakazi na kuboresha maslahi ya walimu nchini, huku ikiitaka CWT kuwa nguzo imara ya weledi, mshikamano na mabadiliko katika sekta ya elimu.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mh. Deusi Sango wakati wa ufunguzi wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambapo serikali imeeleza kuwa mazingira ya kazi ni msingi wa amani ya viwanda na maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Sangu amesema Serikali inaendelea kuheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mikataba ya Kimataifa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), ikiwemo mikataba ya uhuru wa kujumuika, haki ya majadiliano ya pamoja na mashauriano ya utatu, misingi inayochangia ujenzi wa uchumi shindani kuelekea Dira ya Taifa 2050.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *