
Nchini Niger, wiki moja baada ya shambulio la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Niamey, Waziri wa Uchukuzi amezuru eneo hilo. Kanali-Meja Abdourahmane Amadou alienda kutahtmini mfumo wa usalama. Shambulio hilo lilidaiwa na kundi la Islamic State katika Sahel (ISGS), ambayo wiki hii ilitoa maelezo ya toleo lake la matukio.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wawakilishi kadhaa wa mamlaka ya Niger walitembelea mitambo kadhaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori-Hamani huko Niamey. Wiki moja baada ya shambulio hilo, Kanali-Meja Abdourahmane Amadou, Waziri wa Uchukuzi wa Niger, alikuja kuuliza kuhusu uendeshaji wa mfumo wa usalama wa eneo hilo na kutathmini ufanisi wake, kulingana na ripoti iliyorushwa na televisheni ya kitaifa.
Waziri wa Uchukuzi aliandamana na kamanda mkuu wa polisi, mkurugenzi mkuu wa polisi, na mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri wa anga. Uwanja wa ndege una mfumo wa kamera za ufuatiliaji, haswa kando ya ukuta unaozunguka uwanja huo wa ndege. Picha hizo hutumwa kwenye chumba cha ufuatiliaji. Kamera hizo za CCTV (Closed-Circuit Television) zina mchango mkubwa sana katika ufuatiliaji wa mienendo, usalama, na utambuzi wa matukio. ndani na nje ya uwanja wa ndege.
Udhaifu
Katika taarifa iliyotolewa wiki hii, kundi la iskamic State katika Sahel (ISGS) linadai kufuatilia eneo hilo kwa wiki kadhaa ili kubaini udhaifu wa kiusalama. Washambuliaji wanasema waliona lango upande wa mashariki, ambalo mmoja wa magaidi anaripotiwa kupanda ili kufungua kutoka ndani. ISGS hapo awali ilitoa video kutoka kambi ya kijeshi, ikiwaonyesha washambuliaji wakilenga helikopta na ndege mbili ndogo, kabla ya kujirekodi katika sehemu ya raia ya uwanja wa ndege.