Polisi nchini Zambia wamesema kwamba Mvuvi mwenye umri wa miaka 52 amefariki baada ya kushambuliwa na mamba alipokuwa akikimbia kutoshambuliwa na kundi la Tembo katika eneo la Mashariki mwa Zambia. Dean Nyirenda alikuwa anarejea nyumbani kutoka safarini alipokwenda kuvua samaki na wenzake siku ya Jumatano, alipokutana na kundi la Tembo njiani.
Walifanikiwa kuwakimbia Tembo hao, huku Nyirenda akijipata matatani alipokimbilia mtoni akidhania anakwepa kushambuliwa na Tembo bahati mbaya akakutana na mamba katika mto wa Luwangwa. ‘Hapo ndipo alipomshambulia kwa kuumwa mguu wake wa kulia,’ Mkuu wa polisi katika Eneo hilo Robertson Mweemba aliwaambia wanahabari.
Taifa hilo la Kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya tembo ambao mara kwa mara hushambulia watu, hali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi kwa miaka mingi. Polisi wanasema kwamba Nyirenda alifanikiwa kujinasua kutoka kwenye mdomo wa mamba kwa kumgonga mnyama huyo kwa fimbo aliyokuwa ameibeba mkononi.
‘Alijivuta kutoka mtoni,’alisema Mweemba. Wavuvi wenzake wawili ambao walikuwa wanataza kwa mbali, walikimbia kumsaidia na kumbeba kutoka kwa kingo za mto akiwa anatokwa na damu nyingi. ‘Walijaribu kudhibiti eneo ambapo damu ilikuwa inatoka kwa wingi, ila alifariki akiwa njiani kwenda hiospitalini,’ Polisi walisema.
Maafisa wa huduma kwa wanyama pori walifika katika eneo la tukio na kupata kuwa alikuwa ameshambuliwa vibaya na mamba huyo.
Mto Luwanga ambao unapita katika mbuga ya wanyama ya Luwaga Kusini, ni makazi ya mamba aina ya NILE barani Afrika kulinganana takwimu za mashirika ya uhifadhi wa wanyama pori.
Jumla ya vifo 26 vilivyotokana na wanyama pori na ambavyo viliripotiwa mwaka 2023, 15 vilitokana na watu kushambuliwa na mamba – wengi wao katika mto Luwanga – kwa mujibu wa shirika la kijami la Recource Africa.

(Feed generated with FetchRSS)