Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za tiba utalii ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha na kuimarisha sekta ya afya nchini kwa kushirikisha sekta binafsi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt Ayub Kibao amesama hayo leo Ijumaa, Januari 7, 2026 wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya Taasisi ya Kitanzania inayojihusisha na kuratibu na kusimamia matibabu ya binadamu ndani na nje (TanLink Medical Agency sambasamba na uzinduzi wa Kituo cha taarifa cha Hospitali ya Fortis ya nchini India Jijini Dar es Salaam.

Dkt Ayub amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya unakwenda kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha tiba utalii kwa kutoa matibabu kwa wageni kutoka nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanlink Medical Tourism Agency, Dkt Few Magwa amesema lengo la kuzindua ofisi hizo ni kutoa huduma hapa nchini.

Amesema uzinduzi wa ofisi hiyo umekwenda sambamba na ufunguzi wa Kituo cha taarifa kinacholenga kuwasaidia Watanzania kupata taarifa za huduma za tiba kutoka hospitali mbalimbali za nje ya nchi ikiwamo India na China.

Dkt Magwa amesema hatua ya uzinduzi huo unaendana na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha tiba utalii, akibainisha kuwa Tanlink ni miongoni mwa wadau wa sekta binafsi wanaosaidia kutekeleza azma hiyo.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *