
-
- Author, Wanqing Zhang
- Nafasi, BBC Global China Unit and Eye Investigations
-
Muda wa kusoma: Dakika 8
Usiku mmoja mwaka wa 2023, Eric alikuwa akiangalia mitandao ya kijami kwenye simu yake. Siku hiyo alikuw aanafuatilia ukurasa wa mtandao unaoonyesha picha/video za ngono (Pornography) kama alivyokuwa akifanya mara kwa mara, lakini alikutwa na mshangao mkubwa mara tu alivyokutana na video moja iliyokuwa kama anaifahamu.
Aligundua kwamba watu aliyokuwa akiwatazama – wakiingia chumbani, wakijipumzisha na kisha kushiriki ngono kumbe ilikuwa yeye na mpenzi wake. Wiki tatu kabla ya tukio hilo, wawili hao walikuwa kwenye mapumziko katika hoteli moja mjini Shenzhen kusini mwa China, bila kujua kwamba walikuwa wanachunguzwa na kurekodiwa.
Vitendo vyao vya kushiriki ngono vilirekodiwa na kamera za siri ambazo zilifichwa kwenye chumba walicholala. Na baadaye picha hizo za video zilichapishwa kwenye mitandao na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye ukurasa wa mtandao wa kuchapisha video za ngono ambao yeye mwenyewe Eric alikuwa anapenda kuutazama.
Erica (ambalo si jina lake halisia) hakuwa tena mteja wa mtandao huo wa picha za ngono zilizorekodiwa kisiri nchini China, bali alikuwa muathiriwa.
TAHADHARI: Taarifa hii inalugha ambayo huenda ikakukera.
Biashara haramu ya picha za ngono zilizorekodiwa kwa siri almaarufu SPY CAM imekuwepo nchini China kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, japo kurekodi na kutayarisha picha hizo za video kumeharamishwa na ni kinyue na sheria nchini humo.
Lakini katika miaka ya hapo nyuma, suala hili limekuwa kama jambo la kawaida kujadiliw amiongoni mwa wengi katika jamii hasa kwenye mitandao ya kijami – hasa miongoni mwa wanawake – wanaojipa mawaidha ya jinsi ya kutambua kamera za siri zilizofichwa chumbani kwa kutumia kifutio cha kalamu ya mate au penseli. Baadhi wamejitolea kuandamana na wenzaona kukesha kwnenye vyumba vya mahoteli ili kuzuia kurekodiwa.
Mwezi Aprili mwaka jana, kanuni mpya za serikali zilizotolewa zilijaribu kuangamiza tatizo hilo na kulidhibiti – sheria hizo ziliwataka wamiliki wa hoteli kukagua vyumba vya kulała kwa ajili ya kupata na kuondoa kamera za siri.
Lakini tishio hilo la kurekodiwa bila ya kujuwa katika chumba cha kulała kwenye hoteli halijamalizwa kabisa. Idhaa ya dunia ya BBC (BBC World Service) imepata maelfu ya picha za video zilizorekodiwa na kameza za siri kwenye vyumba vya kulała hotelini ambazo zimeuzwa kwa mitandao ya kuonyesha video za ngono.
Video hizi zinatangazwa kwa mtandao wa kijami wa Telegram. Kwa muda wa zaidi ya miezi 8, niligundua tovut sita tofauti ambazo zimefanyiwa matangazo kwa mtandao wa telegram. Miongoni mwa mitandao hii, haya yamedai kuwa na kamera katika vyumba zaidi ya 180 vya Hoteli tofauti a,bazo hazirekodi tu, bali kuchapisha mubashara picha hizo za video kwenye mitandao. Aidha imagunduliwa kwamba nusu ya idadi ya kamera hizo zinafanya kazi kwa saa 24 kwa siku.
Nilifuatilia mmoja ya tofuti nilizozitaja , mara kwa mara kwa muda wa miezi saba na kupata picha zilzizorekodiwa na kamrea 54 tofauti.
Hii ina maanisha kwamba maelfu ya wateja na wageni wanaofika hotelini huenda walirekodiwa katika muda huo, ambapo BBC inakadiria kwamba kutokana na idadi ya wateja hapo ni wengi wlaioathirika. Wengi huenda hawafahamu wala hawajui kuwa wlairekodiwa na kamera hiz za siri.
Eric ambaye ni makzi wa Hong Kong, alianza kutazama picha za ngono zilizorekodiwa kisiri akiwa kijana mdogo. Anasema alivutiwa na jinsi mahusiano yaliyorekodiwa yalivyokuwa kati ya watu ambao hakuwa wanaigiza walichokuwa wakifanya.
‘Kilichonivutia kilukuwa kwamba waliokuwa katika video hizo, hakuwa na ufahamu kwamba wanarekodiwa,’ alisema Eric ambaye kwa sasa ana muri wa miaka 30. ‘Nadhani picha ngono za kawiada zinaonekana sana kuwa watu wenye kushriki huwa wanaigiza, na hazina uhalisia wowote.’
Lakini alishuhudia moja kwa moja wanachohisi wengi ambao wako uoande wa pili wa video hizo – wenye kurekodiwa bila kutoa idhini au kufahamu- alijipata karekodiwa pamoja na mpezi wake ‘Emily’ – na tangu hapo, hahisi tena kwamba video kama hizo za ngono hazifurahisi nafsi yake tena.
Alipomueleza mpenzi wake kuhusu taarifa hiyo,kwamba hoteli walipolala walirekodiwa kisiri, na picha hizo kuhaririwa na kuchapishwa mitandaoni ambapo watazamaji walipata fursa ya kuwatazama wakiwa na mahusiano yao kw asaa nzima, alidhani kwamba ni mzaha. Ila alipotazama picha hizo za video kwwneye mtandao wa telegram, alishtuka sana.
Emily alishtuka kabisa kuona video hiyo na kuhofia kwamba huenda ikatzamwa na wafanyakazi wenzake au hata jamaa zake nyumbani. Baada ya hapo, wawili hao hawakuzungumza kw awiki kadhaa.
Kwa hivyo sekta hii ya biashara – ambayo inawadhulumu wapenzi wasiokuw ana habari yoyote kuhusu kurekodiwa kwa siri – inafanya vipi kazi zake na ni nani anayesimamia biashara hiyo?
Nilijifanya kama mteja na kulipia kupata huduma ya tovuti inayotangaza video za ngono mubashara. Kila mwezi nilikuwa nalipa dola 65, sawia na Pauni 47 ama Yuan 450.
Nilipoiingai kwenye mtandao huo, nilikuwa na uwezo wa kuchagua katika chaneli tano ambazo zilikuwa zinatangaza mubashara pica za ngono, kila mmoja ikioneysha picha kutoka kwa kamera za siri zilzizowekwa kwatika vyumba vya kulała kwenye hoteli kadhaa. Picha hizo zilianza kurekodiwa punde tu, mtu anapoingia ndani ya chumba kwa kutumia kadi ya kufungua mlango na kemera zinaanza kufanya kazi .

Katika mtandao wa Telegram – ambao umepigwa marufuku China, ila bado unatumika sana kwa shughuli ambazo si halali – AKA ilitangaza matangazo ya mubashara ya video za ngono. Chaneli moja ya Telegram ilikuwa na wateja zaidi ya 10,000 katika muda ambao tulifanya uchunguzi wetu.
Vile vile kuan hifadhi ya vodeo za ngono kwenye mtandao huo huo wa Telegramkwa wale wanaotaka kutazama baadaye kwa malipo. Nilikuw anaweza kuona kwamba kuna vido zaidi ya 6,000 ambazo zimehofadhiw apale ambazo huenda zilirekdoiwa 2017.
Wateja wa AKA wanaweza kutoa maoni yao kwenye chalei hiyo ya Telegram, wanapoendelea kutazama video hizo zawageni wanaoigia katika vyumba vya hoteli – wakikagua jinsi miili yao ilivyo, wakiwasema kuhusu mazungumzo yao na hata kufanya Tathmini ya mbinu zao za kujamiaana.
Wanashereheka wakati ambapo wapenzi ama wanadoa wanapoanza kushirki ngono – na hulalamika ikiwa wapenzi hao watazima taa, wakikasirika ni kwa nini wanafanya mambo yao kwenye giza. Wanawake hupewa jina la ‘hawara’ na mengine mengi ya kuwadhalilisha.
Tumefanikiwa kupata moja ya kamera hizo za siri katiak chumba hiki kilichowekwa katika hoteli ya Zhengzhou iliyopo katikati mwa hina, hili iliifanikishwa kwa kuweka pamoja mambo muhimu , tiloyoyapata kutoka kwa watejwa wa mitandao hiyo, mtandao w akijamii na utafiti wetu.
Watafiti waliokuwa katika Eneo hilo, waliweza kuingia katika chumba hicho cha hoteli, na kuipata kemra – lensi yake ilikuwa imeangalizwa kwa kitanda na ilikuwa imefichwa kwenye mfumo wakuleta hewa safi chumbani na waya zake zilikuwa zimeunganshwa na mfumo wa stima wa ndani ya chumba.
